Saturday, 21 April 2018

Beckham atoa neno kuhusu Wenger kutangaza kustaafu kuifundisha Arsenal

Wadau mabalimbali wa soka duniani wameendelea kutoa maoni yao tangu hapo jana (Ijumaa) Arsene Wenger alipotangaza kustaafu kuifundisha Arsenal mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaji mwenye heshima kubwa Uingereza na duniani, David Beckham ametoa maoni yake kuhusu kocha huyo huku akidai kuwa Wenger alikuwa hapati heshima yake iliyokuwa inastahili kwenye soka japo amefanya makubwa.
Beckham amesema hayo kupitia mtandao wa Instagram huku akiongeza kuwa kocha huyo alisaidia kuleta ushindani mkubwa kwenye ligi kuu hasa kwa klabu ya Manchester United.
Kupitia mtandao huo, Beckham ameandika:
Labda mtu huyu sasa atapata heshima anayostahili kwa miaka 22 ya kuleta wachezaji wakubwa, soka kubwa na ushindani mkubwa kwa sisi @manchesterunited kwenye ligi kuu. Sasa ni wakati wa kusherehekea kila kitu ambacho Arsene alitoa kwa klabu ya soka ya Arsenal @arsenal
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: