Monday, 30 April 2018

Baada ya Seduce Me, Alikiba awang’ata sikio mashabiki wake

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wake wanasubiria wimbo mpya.

Hata hivyo ameeleza kuwa katika ukimya wake amejitahidi kufanya mambo mengi kwa ajili yao. Moja ya vitu alivyofanya ni pamoja na kuleta bidhaa yake mpya ya kinywaji (energy drink), MOFAYA.
“Kitu ambacho naweza nikawaeleza tumefanya mambo mengi katika ukimya wangu, najua watu walikuwa wanasubiria wimbo mpya itoke lakini pamoja na hayo kuna vitu vipya nimejihusisha navyo katika biashara ambayo naifanya,” amesema Alikiba.
Wimbo wa mwisho kwa Alikiba kutoa ni Seduce Me ambao ulitoka Augost 25, 2017, hadi sasa ukiwa na views zaidi milioni 9.4 katika mtandao wa YouTube. Baada ya wimbo huo aliweza kushirikishwa na Abdu Kiba katika wimbo unaokwenda kwa jina la Single

No comments:

Post a Comment