Klabu ya soka ya Azam FC imeeleza kuwa mlinzi wake David Mwantika, anaendelea vizuri baada ya kupata hitilafu ya mwili wakati wa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar.
Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankema, anayeshughulikia taratibu za matibabu ya Mwantika amesema kuwa beki huyo anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Tunamshukuru Mungu David anaendelea vizuri na matibabu na yupo kwenye hatua za kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu kutoka kwenye tatizo lililompata juzi,” alisema.
Mwantika alizimia dakika ya 64 na kupatiwa matibabu ya awali kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakhem na kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, na baadaye Muhimbili (MNH) ambako anaendelea kupata matibabu.
Aidha Dkt. Mwanandi amesema taratibu zinazofanyika kabla ya mchezaji huyo kuruhusiwa ni kufanyiwa uchunguzi wa moyo ili kufahamu kama ana tatizo hilo kwaajili ya matibabu zaidi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: