Friday, 13 April 2018

AZAM KUISHUSHA YANGA MPAKA NAFASI YA TATU LEO


Kikosi cha Azam FC kinashuka dimbani jioni ya leo kucheza dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Azam wanahitaji pointi tatu ili waweze kuishusha Yanga kwa muda kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo itakuwa ina michezo miwili nyuma.

Mpaka sasa Azam wana alama 45 huku Yanga wakiwa na 47 hivyo endapo watashinda leo watapanda mpaka nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 48 huku Yanga ikishuka namba tatu ikisalia na alama zake 47.

Tayari kikosi chao kipo mjini Mlandizi tayari kwa mchezo huo ambao uliahirishwa jana kutokana na mvua kunyesha.

Mchezo huo uliahirishwa baada ya Uwanja wa Mabatini kujaa maji kufuatia mvua kubwa kunyesha jana.

Mechi hiyo itapigwa leo saa 10 kamili jioni 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: