Aunt Ezekiel : Inatosha sasa Kumlilia Kanumba - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 12 April 2018

Aunt Ezekiel : Inatosha sasa Kumlilia Kanumba

Aunt Ezekiel

STAA wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa hakuna sababu ya kulia kila siku kuhusiana na kifo cha aliyekuwa staa wa filamu Steven Kanumba, badala yake waige mfano wake ili tasnia hiyo izidi kusonga mbele.

Akizungumza na gazeti hili, Aunt alisema mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika alipokuwa amefika yeye.

“Najua wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja,” alisema Aunt.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done