Askofu Mkuu Zachary Kakobe aitwa Uhamiaji Jumatatu kuhojiwa juu ya uraia wake


Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar-Es-Salaam, imemwandikia barua Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, kumwita kwa ajili ya mahojiano.

 Askofu Kakobe ametakiwa kufika katika ofisi hiyo, Jumatatu 9.4.2018 saa 4 asubuhi, na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ili kuhojiwa juu ya uraia wake.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Askofu Kakobe amethibitisha kupokea barua hiyo, na kusema kifupi tu kwamba, atakwenda kwenye mahojiano hayo.

Tukio hili linakuja baada ya sekeseke kati ya Askofu huyo na TRA, kuhitimishwa tarehe 20.2.2018, siku ambayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alipotoa taarifa kwa umma juu ya uchunguzi wao; na baadaye kusema mjadala huo umefungwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: