Matumaini ya Klabu ya Arsenal kutinga ‘Big Four’ msimu huu wa 2017/18 kunako Ligi Kuu nchini England (EPL) yanazidi kupotea ambapo leo imekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

Kwa sasa Arsenal inahitaji ushindi wa mechi zake tano zilizobakia huku ikiombea klabu ya Chelsea na Spurs kupoteza michezo angalau mitatu mitatu ili Arsenal iingie kwenye Big Four.

Kwa sasa Arsenal wamesalia kwenye nafasi ya sita wakiwa na alama 54 nyuma ya Chelsea alama 60 na Spurs alama 67 na timu zote zina michezo mitano mkononi ya ligi.

Bila shaka hali ni ngumu kwa Arsenal pengine kuliko Chelsea, lakini ahueni kwa Arsenal ni kwamba bado wapo kwenye michuano ya Europa hivyo endapo watashinda taji la michuano hiyo basi kwa sheria mpya watashiriki michuano ya klabu bingwa mwakani moja kwa moja.

Hii ni rekodi mbaya kabisa kwa klabu ya Arsenal ambapo inakuwa klabu ya kwanza kubwa kupoteza michezo mitano mfululizo ugenini bila kupata hata sare, kwenye ligi hiyo kubwa kabisa duniani
Share To:

msumbanews

Post A Comment: