Thursday, 19 April 2018

Aliyepanga shambulizi la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani akamatwa

Moja kati ya matukio makubwa ya kigaidi kuwahi kutokea nchini Marekani ni lile la Septemba 11, 2001 lililolipua majengo pacha ya World Trade Center na jengo la Pentagon, shambulio ambalo lilitekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda lililokuwa likiongozwa na Osama Bin Laden. Hatimaye moja ya watu waliohusika na upangaji wa tukio hilo amekamatwa.
Mohammed Haydar Zammar katikati kwenye picha
Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Mohammed Haydar Zammar raia wa Ujerumani amekamatwa nchini Syria na Wanamgambo wa Kikurdi wanaofanya kazi ya kulinda amani kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa shirika la utangazaji la Reuters, umeeleza kuwa taarifa zilizotolewa na msemaji wa kundi hilo zinadai kuwa Zammar amekiri kufanya hivyo baada ya kufanya naye mahojiano kwa muda mrefu.
Zammar pia anashutumiwa kutekeleza mashambulizi mengine ya kigaidi nchini Ujerumani kama lile la uwanja wa Hamburg mwaka 1990.
Imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 3000 walipoteza maisha kwenye shambulio hilo la kigaidi la Septemba 11, 2001. Hata hivyo Marekani ilifanikiwa kumuangamiza kiongozi wa kundi la Al-Qaeda, Osama Bin Laden mwaka 2014 .
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: