Wednesday, 25 April 2018

Alikiba - Siwezi kuruhusu maisha ya kiki au kufanya jambo ili kutaka kuzungumziwa na watu.

Msanii wa bongo fleva Alikiba ambaye hivi karibuni amefunga ndoa na Binti wa Kimombasa ajulikanae kwa jina la Bi. Amina Khalef amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hawezi kuruhusu maisha ya kiki au kufanya jambo ili kutaka kuzungumziwa na watu.

Alikiba amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Nirvana Deogratius Kithama na kusema watu ambao wanafanya kiki wacha waendelee na hizo kiki ila yeye hawezi kufanya hivyo kwa kuwa anatambua watu wake wengi na mashabiki walitokea kumkubali na kumpenda kutokana na heshima yake hiyo haoni sababu ya kuanza kuhangaika kuivunja heshima ambayo amejijengea kwa muda mrefu.

"Ni kweli wapo watu wanafanya sana kiki ila mimi siwezi hilo, wanaofanya hivyo wacha waendelee kufanya ila mimi sioni sababu kwa kuwa mimi watu wengi wametokea kunipenda na kupenda kazi zangu kutokana na heshima ambayo nimekuwa nayo, hivyo siwezi kuivunja heshima yangu kwa kiki na nitaendeleza haya maisha yangu mpaka siku nakufa" alisisitiza Alikiba

Alikiba April 29, 2018 anatarajia kufanya sherehe ya harusi yake jijini Dar es Salaam na tetesi zilizopo baada ya sherehe hiyo wawili hao wanatarajia kwenda nchini Italia kwa ajili ya fungate.

No comments:

Post a Comment