Alichokizungumza Askofu Kakobe baada ya kuhojiwa Idara ya Uhamiaji

Askofu Mkuu wa Kanisa Full Gospel Bibble Fellowship, Zachary Kakobe baada ya kuitwa na kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji Jumatatu hii ameeleza alivyohojiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutoka kuhojiwa katika Ofisi za Idara ya Uhamiaji amesema kuwa kubwa alilohojiwa ni kuhusu uraia wake.
Wito kutoa maeleza kuhusu uraia wangu kwahiyo mahojiano yote yalikuwa yamebase kuhusiana na uraia kwa maana nyingine ni kutoa maelezo yanayohakikisha kwamba mi ni raia wa nchi hii sasa bibila inasema katika Mithali 28;1 muovu anakimbia hata ajafuatwa na mtu lakini mwenye haki ni jasiri kama Simba,” amesema Kakobe.
Sasa mimi sina uovu wowote ni Raia wa nchi hii kwahiyo nimetoa maelezo yote ya kina na ambayo yako wazi kabisa kwamba mimi ni raia wa hapa.”
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: