Saturday, 14 April 2018

Ali Kiba kufunga ndoa Aprili 19


Mashabiki wa mkali wa Bongo Flava, Ali Kiba waliamini kabisa mrembo Jokate Mwegelo ndiye angekuwa mke halali wa supastaa huyo, lakini mambo yamekuwa tofauti.

Habari za kuaminika ni kuwa, Kiba anatarajiwa kufunga ndoa na mpenzi wake Amina Khaleef, Alhamisi ijayo mjini Mombasa.

Ndoa ya Kiba na Khaleef ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki, ambapo sasa mambo ndio yamekuwa moto huku amsha amsha za harusi hiyo zikipamba moto.

Imeelezwa kuwa, mpango mzima wa harusi hiyo unasimamiwa na rafiki wa karibu na Kiba, Sultan Joho ambaye ni Gavana wa kaunti ya Mombasa.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, ndoa hii itafanyika hapa Mombasa na nyingine kule Dar es Salaam. Kwa sasa Kiba yuko nchini China kukamilisha mambo madogo madogo ya nyumbani, lakini hapendi habari za hii ndoa kujulikana.

“Ndoa itafungwa Aprili 19 hapa Mombasa na kule Dar itakuwa Aprili 29, shughuli nzima inasimamiwa na marafiki zake wa karibu akiwemo Joho (Sultan),” kilisema chanzo chetu.

Hivi karibuni mkali mwingine wa Bongo Flava, Ambwene Yesaya a.k.a AY alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku, ambapo alifanya sherehe mbili moja kule Kenya na nyingine hapa Tanzania.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: