Ajali ya ndege Algeria yauwa 257


Ndege ya kijeshi ya Algeria iliyokuwa imebeba wanajeshi imeanguka Jumatano asubuhi na kuuwa watu 257.

Maafisa wamesema kuwa ndege hiyo imeanguka karibu na kituo cha ndege za kijeshi cha Boufarik muda mfupi baada ya kuruka.

Wizara ya ulinzi ya Algeria imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea kwenye eneo la Tindoufkusini mashariki mwa taifa hilo.

Mpaka wakati huu sababu za kuanguka ndege hiyo hazijaweza kufahamika.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: