Tuesday, 24 April 2018

Ado Shaibu afunguka ishu ya 'kufichwa Zitto Kabwe'


ACT Wazalendo kupita kwa Katibu wa Uenezi wa Chama hicho Ado Shaibu kimefunguka na kuweka wazi kuwa Kiongozi Mkuu wa chama hicho Mhe. Zitto Kabwe hajafichwa kama ambavyo watu wanasema bali sasa hivi ameongezewa ulinzi na mienendo yake inaangaliwa kwa kina na idara ya ulinzi na usalama.

Ado Shaibu amedai kuwa zipo taarifa zinaenea kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali kuwa kiongozi huyo anaweza kuuawa na kusema ndiyo sababu kubwa ambayo imepelekea sasa kulindwa kwa daraja la juu kabisaa la ulinzi.

"Ukisikia kwamba kiongozi wenu anataka kushambuliwa, kudhuriwa au kuuwawa ni muhimu kuyapa uzito sana maneno hayo kwa hiyo sisi tumechukua hatua kadhaa kwanza ndugu Zitto alikuwa na mkutano wa hadhara Kigoma Ujiji alikuwa anataka kuzungumzia masuala yanayoendelea nchini kuhusu ripoti ya CAG lakini alitaka kuwaeleza watu wa Kigoma wapi amefikia kuhusu suala la watu wa Kigoma kunyanyaswa uhamiaji na kutaka maoni ya wananchi kwa hiyo mkutano wenyewe huo ulizuiwa na sisi tulikuwa na mkutano wa ndani wa chama kutokana na mambo haya yanayoendelea tukaamua ni bora tusimamishe kikao hicho" alisema Shaibu

Ado Shaibu aliendelea kusema kuwa

"La pili kiongozi wa chama ameongezewa ulinzi na idara ya ulinzi na usalama ya chama kuhakikisha kwamba anakuwa salama na kuchunga mienendo yake ndiyo maana utaona baadhi ya magazeti yanasema Zitto Kabwe amefichwa, ndugu Zitto ni kiongozi hawezi kufichwa lakini mienendo yake sasa inadhibitiwa na idara ya ulinzi na usalama ya chama awe wapi, muda gani na kwanini, awe ndani ya nchi, nje ya nchi hayo ndiyo mambo ambayo idara yetu ya ulinzi na usalama inayapa kipaumbele kikubwa, kwa hiyo kiongozi sasa analindwa kwa daraja ya juu" alisisitiza Ado Shaibu

Baada ya Zitto Kabwe kuonekena ameikomalia sana ripoti ya CAG hasa zaidi kuhusu 1.5 Trilioni ambayo haileweki imetumikaje zilianza kusambaa taarifa mbalimbali kuwa kiongozi huyo naye anaweza kushughulikiwa na watu wasiojulikana.

No comments:

Post a Comment