Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari mmoja wa Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Telegram.

Hatua ya kuwashikilia watu hao ni kufuatia agizo la Rais JPM la kukemea vikali watu wa namna hiyo wanaohamasisha maandamano huku akidai kuwa Tanzania ni nchi ya amani, hivyo maandamano hayaruhusiwi kufanyika..

“Wapo watu wangependa nchi hii kila siku tuwe na migogoro, Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli, wangependa kila siku tuko barabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku, wao wanataka wabaki wanaandamana kule. 

Nitasema ngoja waandamane wataniona. Kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri. 

Niliapa kwa katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani.” Amesema Rais John Pombe Magufuli.

Rais alizungumza hayo mnamo mwezi Machi mwaka huu pindi akijaribu kukemea harakati za maandamano zinazoendelea nchini, ambapo inadaiwa kuwa kuna watu wasiojulikana wanahamasisha kufanyika kwa maandamano Aprili mwaka huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: