Zaidi ya wanachama 90 kutoka Act Wazalendo na Chadema Arusha wajiunga na Ccm

Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg. Abraham Mollel  Akipokea kadi za wafuasi wa chadema waliojiunga na Ccm mapema leo asubuhi.

Baadhi ya Kadi zilizorudishwa na wafuasi wa chadema mapema leo.

WANACHAMA Zaidi ya 90 katika Wilaya ya Arusha Mjini Mkoani Arusha, kutoka Act Wazalendo na  chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wamejiunga na chama cha Mapinduzi
Akipokea wanachama hao mapema leo Asubuhi Katibu Mwenezi wa  Arusha Mjini Ndg. Abrahamu Molle amesema 

"Leo tumepokea wanachama zaidi ya 90 wakiwa wameongozana na Diwani wa Osunyai wafuasi hawa wa chadema wameniletea na katiba yao pamoja na muhuri kwa hiyo kwa sasa ile ofisi ya Chadema Arusha mjini haina tena wanachama wala viongozi kwa hiyo nitoe tu rai kwa  ndugu yangu Lema,Meya Kalist Lazaro na Bananga kuwa sasa watuachie arusha yetu tufanye siasa za amani na utulivu maana mmezoea maandamano"

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Bw. John Laizer  ambaye amehamia kutoka CHADEMA, alisema wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa na mwelekeo wake. Alisema wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero za wananchi.

Alisema amekaa upinzani kwa miaka 13 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya malipo yenye jina lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: