Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ya Botswana, umemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa wenyeji kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Township Rollers ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kwanza mapema kabisa kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye.

Baada ya bao hilo la kuongoza kwa Rollers, Yangan waliendelea kupambana ambapo katika dakika ya 30, mshambuliaji Obrey Chirwa aliweza kufunga bao la kusawazisha, kufuatia kazi nzuri ya Papy Tshishimbi aliyetoa pasi kwake.

Mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza, matokeo yalikuwa ni 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu, ambapo nyavu hazikuweza kutikisika mapema, ambapo ilichukua muda mpaka zikasalia dakika 7 zikisalia kuelekea mwishoni mwa mchezo, Sikela akafunga bao la pili kwa Rollers katika dakika ya 83.

Mpaka dakika 80 zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Yanga kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Gaborone Botswana, ambapo watabidi washinde mabao zaidi ya mabao mawili kwa sufuri ili waweze kusonga mbele.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: