Wema Sepetu : Rc Makonda ni zaidi ya Mfalme ameletwa na Mungu - MSUMBA NEWS BLOG

Friday, 2 March 2018

Wema Sepetu : Rc Makonda ni zaidi ya Mfalme ameletwa na Mungu


Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amefunguka na kudai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameletwa duniani na Mungu kwa lengo la kusaidia watu nasio vinginevyo.
Wema ametoa kauli hiyo mara baada ya Mhe. Makonda kuonesha nia ya kumsaidia kumsafirisha kijana Ahmed Albaity kwenda nchini China kwa lengo la kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa aliokuwa nao wa kupooza mwili mzima.
"Nikisema 'RC' wangu ni mtumishi wa Mungu basi namaanisha, mimi 'sometimes' nasema uliletwa duniani kuja kufanya ya Mola wako tu. Mungu azidi kukubariki 'my RC you are just like a guardian angel', ipo siku wataelewa tu. 'I got a Good Feeling about Ahmed and Inshallah God will work a miracle, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho", amesema Wema Sepetu.
Kijana Ahmed Albaity alipooza mwili wake mnamo 2007 baada ya kucheza vibaya michezo ya kujirusha 'dive' katika bahari na kwa bahati mbaya alikosea na kujipiga kichwa chini ambapo ilipelekea kupata matatizo yote hayo mpaka sasa.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done