Waziri wa mambo ya ndani, Dr Mwigulu Nchemba ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma mjini, mkoani humo ambapo ndipo patajengwa   Ofisi za makao makuu ya Idara ya uhamiaji.

Tayari Rais Dr John Magufuli ameshatoa kwa idara hiyo Sh bilioni 10  na kwamba ujenzi wa ofisi hizo  unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza wakati alipotembelea ofisi hizo leo, Dr Mwigulu amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuwapa fedha hizo ambzo ni Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji.

Amesema tayari kwasasa  eneo kubwa lenye mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa idara hiyo.

"Eneo limeshapatika kubwa la kutosha la kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo muheshimiwa Rais amesemea wakati anatuhaidi kutupa fedha hizi  sasa tumepata eneo la kutosha ambalo lipo karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa,zimamoto na ofisi zingine za serikali ambapo itasaidia kama mtu akifika uhamiaji anaweza kupata zingine ambazo zipo karibu". Aliongeza waziri mwigulu.

Waziri mwigulu ametoa rai kwa idara ya uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma kwani kama wangefata kupata fedha katika bajeti ya wizara ingechukua mda mrefu kupatikana fedha hizo hivyo kufanya kazi kwao vizuri kunamfanya hata yeye kuwa waziri wa mamboya ndani mzuri.

Naye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dr Anna Makakala amemshukuru muheshimiwa Rais Dr John magufuli kwa  kuwapa fedha hizo kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote.

"Sisi kama idara tunajukumu la kufata taratibu zote kwa haraka iwezeka nanvyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liweze kukamilika kwasababu kama fedha ni zipo".alisema Dr Anna.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: