Wastara : Mange Kimambi Anacheti cha Mirembe - MSUMBA NEWS BLOG

Wednesday, 14 March 2018

Wastara : Mange Kimambi Anacheti cha Mirembe


Msanii wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo maana anakurupuka katika baadhi ya mambo. 
Wastara amesema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI na kusema kuwa Mange Kimambi alizusha juu ya Cannula aliyowekwa mkononi na kusema alijiwekea mwenyewe, Wastara amesema kuwa mbali na kuzusha huko lakini dada huyo alikwenda mbali mpaka kuwauliza madaktari wa hospitali aliyokuwepo kama anatibiwa hapo. 
"Mange Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe" alisema Wastara 
Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha. 
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done