Wanne wafariki dunia na 20 wajeruhiwa MbeyaWatu wanne wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas kugongana na lori jana Machi 8, 2018 katika eneo la Igawa wilayani ya Mbarali mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 170 DKS lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe kugongana na lori lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lililokuwa limebeba kontena.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,  chanzo cha ajali ni dereva wa basi aliyekuwa akijaribu kulikwepa tawi la mti lililokuwa limeegeshwa barabarani kama ishara ya kuonyesha kuwepo kwa gari bovu mbele yake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: