Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika leo katika ukumbi wa karimjee.

Mstahiki Meya wa  Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote  jijini  kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwa hawana  ndugu.
Meya Mwita ametoa kauli hiyo leo, kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji, kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.
Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo sasa ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao. Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema Meya Mwita.
Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali
Share To:

msumbanews

Post A Comment: