Baadhi ya watu waliotangazwa kwenye orodha ya wanachama wa ACT Wazalendo waliokihama Chama hicho na kuhamia CCM wamekana kuhama kuhama chama hicho, orodha hiyo imesomwa leo mbele ya waandishi wa habari na Kalumuna Ernest aliyejitambulisha kuwa Katibu wa chama hicho.

Hii ni Mara ya pili kwa ndugu Kalumuna kutangaza kukihama Chama cha ACT Wazalendo ambapo mara ya kwanza alitangaza kufanya hivyo kwenye kampeni za CCM katika Jimbo la Kinondoni. Hata hivyo Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Afisa Habari wake Abdallah Khamis alieleza kuwa Chama hicho kilishamuondoa kwenye ukatibu wa Mkoa na Kamati Kuu miezi mingi nyuma.
Akizungumza na mwandishi wetu , mmoja wa watu waliotajwa Kwenye orodha ya leo iliyosomwa na Kalumuna, Robert Kihiri ambaye alitajwa Kama Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Ubungo amesema “Wapuuzeni hao watu, ni wahuni. Wamenifuatilia mimi kwa simu hadi kwangu wamefika kunishawishi nijiunge CCM, nimekataa. Mimi bado ni mwanachama wa ACT Wazalendo na sina Shaka na mwenendo wa Chama chetu. Sijakihama Kama wanavyodai,” amesema Robert Kihiri.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: