Tokeo la picha la
Godfrey Mutabazi
Tume ya Mawasiliano nchini Uganda (UCC) imetangaza kuvifungia vituo 23 vya redio kwa kurusha matangazo ya waganga wa kienyeji.
Taarifa za kufungiwa kwa vituo hivyo 23 limetolewa jana jioni na mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.
Mutabazi ameshutumu vikali vituo hivyo vya redio kwa kitendo cha kuwaruhusu waganga wa kienyeji kutangaza matangazo yao na kuvunja sheria ya uchawi ya kifungu cha pili.
Redio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kwa njia ya simu.
Akiongea na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Msemaji wa Tume ya mawasiliano Uganda, Pamela Ankunda amesema kuwa kuruhusu matangazo ya waganga wa kienyeji ni kosa kisheria.
Kwa kuwaweka hewani matapeli wanaojiita waganga wa kinyeji, wakitumia mbinu mbali mbali wakiwa hewani ili kuwatepeli wananchi. Kwa mfano kwa kuwalaghia wananchI kwamba ukituma fedha hizo kwa njia ya simu ya mkononi utapata utajiri, baada ya kutuma kesho yake utapata mamilioni ya fedha chini ya kitanda chako.Hivyo tumetumia sheria ya kuwajibisha radio hizo na kufunga FM Radio 23 baada ya kusikiliza matangazo hayo.“amesema Bi. Ankunda .
Hata hivyo, hatua hiyo imekuja kufuatia muendelezo wa maonyo kwa miaka miatatu tangu juu ya vyombo vya habari hususani Redio na Runinga kutokujihusisha na matangazo ya waganga wa kienyeji.
Baadhi ya vituo vilivyofungiwa ni kituo cha Metro FM na Dembe FM vyote vya jijini Kampala na vingine ni kutoka mikoani nchini humo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: