Video ya utupu ya Eric Omondi yazua gumzo Kenya, Mashabiki wataka ashitakiwe - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 1 March 2018

Video ya utupu ya Eric Omondi yazua gumzo Kenya, Mashabiki wataka ashitakiwe

Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Eric Omondi amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuachia video ikimuonesha akiongelea kwenye mto akiwa mtupu na watoto wadogo.
Eric Omondi
Kwenye video hiyo Omondi anaonekana akioga akiwa mtupu huku watoto wadogo ambao kwa muonekano wao ni makadirio ya chini ya miaka 10.

Baada ya kuposti video hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, alianza kushambuliwa na mashabiki wake na wanaharakati nchini Kenya wakitaka aburuzwe mahakamani kwa kujibu mashtaka ya kuwadhalilisha watoto wengine wakimsapoti kwa kusema kuwa anaenzi tamaduni.
Hata hivyo, tayari Eric Omond ameomba msamaha kwa kitendo hicho mapema asubuhi ya leo kwa kusema kuwa amekosea kuweka video hiyo mtandaoni.
I have been a comedian all my life… Many are the times that I have errored… Today was one of those days. I have offended so many. I did not in any way intend to offend anyone, I AM DEEPLY SORRY FOR THAT,“amesema Eric Omondi
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done