Sunday, 25 March 2018

update : Ajali ya gari yaua watu 24 Pwani

Imeelezwa kuwa watu 24 wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa vibaya baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata ambapo amesema majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Kamanda Likwata amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 25, 2018 eneo la Mparanga wilayani Mkuranga ambapo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Chanzo:Mwananchi

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: