Saturday, 31 March 2018

Uongozi wa Singida United wakanusha taarifa hii

Uongozi wa klabu ya Singida United umekanusha taarifa za mchezaji wao, Danny Usengimana kuondoka kikosini na kutimkia kwao Rwanda sabababu iliyotajwa kuwa ni madai ya mshahara.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa timu hiyo, Festo Sanga, amesema mchezaji huyo hajaondoka sababu ya madai ya mshahara na badala yake amerudi kwao Rwanda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia.

"Si kweli kuwa anadai pesa, amerudi kwao mara moja kurekebisha matatizo ya kifamilia, hivyo baadaye atarejea kujiunga na wenzake kikosini" alisema Sanga.

Taarifa za ndani kutoka Singida United zinaeleza kuwa mchezaji huyo ameondoka klabuni kutokana na kutolipwa pesa zake za mshahara hivyo kusababisha atimkie kwao Rwanda.

Usengimana ameondoka Singida ikiwa imesalia siku moja ya leo Jumamosi kabla ya kibarua cha mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: