Umoja Wa Rudisha Uzalendo (RUTA) Waandaa Maandamano ya Kupongeza Juhudi Za Rais Magufuli


WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam  kupitia Umoja wa Rudisha uzalendo Tanzania (RUTA) umepongeza juhudi za Rais Dk.John Magufuli na watendaji kazi wake katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini huku wakitangaza kufanya maandamano ya amani Aprili 12 mwaka huu.

Hayo yameelezwa jana  na Mratibu wa umoja huo Charles Masele  jijini Dar es Salaam ambapo alisema  kuwa wananchi wengi wamevutiwa na wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli, hivyo katika kumpongeza wameandaa maandamano ya amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yatakayofanyika Aprili 12 mwaka huu kuanzia Karume hadi viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa moja hadi saa tano asubuhi .

Wakizungumza zaidi  wadau hao walisema hawana budi kuunga mkono juhudi za Rais kwani huduma nyingi zimeboreshwa zikiwemo miundombinu, afya hasa kwa akina mama na elimu ambayo hutolewa bure, pia mikopo ya elimu ya juu ambayo hutolewa kwa wanafunzi wa hali ya chini.

Aidha wameeleza utiifu wa Rais na watendaji wake wa serikali na taasisi binafsi kwa namna wanavyothamini na kuhudumu kwa haki na usawa hivyo wameona ni vyema kumuunga mkono na kumuombea.

Pia umoja huo umewataka vijana na watu wa kada mbalimbali kuunga mkono juhudi hizo kwani zinafanywa kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na baadaye.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: