MUME wa staa wa Mduara B0ng , Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambaye alifunga naye ndoa miezi kadhaa iliyopita, Ashiraf Uchebe amefunguka kuwa, tangu aingie kwenye uhusiano na mwanamama huyo hadi sasa , hajawahi hata kumzibua kofi.

Uchebe aliliambia Ijumaa kuwa, watu wengi wanamuona yeye kama baunsa ambaye kila wakati anaweza kupiga mtu, jambo ambalo si kweli kwani anampenda mno mkewe huyo hivyo hawezi kumtandika makofi.

“Watu wengi wananiona kama mtu wa kupigapiga, lakini siwezi kumtandika mke wangu hata siku moja,” alisema Uchebe mwenye umbo dogo ukilinganisha na Shilole.
Kwa upande wake Shilole alipoulizwa kuhusu habari zilizoenea mitandaoni za kupokea kipondo kutoka kwa Uchebe alisema hakuna ishu kama hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: