Friday, 16 March 2018

TRAFIKI AGONGWA NA GARI AKIONGOZA MATAA YA SAYANSI DAR


OFISA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye jina lake halijatajwa amepata ajali ya kugongwa na gari wakati akiongoza magari katika makutano ya Barabara yaliyopo Kijitonyama maarufu kama Mataa ya Sayansi jijini Dar.

Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari jijini humo.

“Hii ni taarifa ya kusikitisha kuhusu ofisa wa jeshi la polisi aliyekuwa kazini akiongoza magari pale Mataa ya Sayansi, amegongwa na gari na madereva wasiozingatia sheria za usalama barabarani, amevunjika mkono kwenye kiwiko na juu ya kiwiko, pia ameumia kichjwa kwani alianguka chali.

“Muda mfupi uliopita nimetoka kumuona hospitali anaendelea vizuri. Niwaombe madereva wazingatie sheria za barabarani. Bila askari wa usalama barabarani tutashindwa kwenda makazini na walioko makazini watashindwa kurudi nyumbani,” alisema Mambosasa.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: