Tanzia : Mchezaji wa Simba afariki - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 1 March 2018

Tanzia : Mchezaji wa Simba afariki


Mchezaji wa Zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam.
Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.
"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki", amesema Manara.
                                        Marehemu Arthur Mambeta  enzi za uhai wake.
Uongozi wa Msumbanews Blog kwa pamoja unawapa pole wadau wa soka nchini, familia ya marehemu na klabu ya Simba kwa kuondokewa na mtu muhimu. 
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done