TAASISI YA WE CARE TANZANIA WAMTUNUKU CHETI CHA HESHIMA MBARAZA UVCCM TAIFA NDG. OMEGA THOBIAS


Mkurugenzi wa Taasisi ya WE CARE TANZANIA iliyopo Jijini Mbeya Bi. Elizabeth Maginga amemtunuku Cheti cha Heshima Ndugu Omega Thobias- Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Njombe. 

Bi. Elizabeth na Taasisi yake waliandaa Tamasha kubwa mwishoni mwa mwaka 2017 la kuhamasisha Jamii kuhusu Uchangiaji Damu salama kwa hiari kwa kusaidiana na Benki ya Taifa ya Damu Salama ambapo Bw. Thobias alishiriki kikamilifu. 

We Care Tanzania pia wamemtunuku Cheti hicho Miss Mbeya 2017 Miss Patricia Richard,  Mshiriki wa Shindalo la Miss Mbeya 2017 Miss Evangelina Peter na Mchekeshaji maarufu Jijini Mbeya aitwaye Kashili (Chance Kashililika). 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: