Monday, 12 March 2018

Shahidi : Chumbani wa wema nilikuta sigara wala sio Bangi

MJUMBE wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi msanii wa filamu, Wema Sepetu, Steven Alphonce ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili staa huyo, amedai wakati wa upekuzi walikuta kipande cha sigara wala si bangi.

Alphonce amesema hayo leo Jumatatu, Machi 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili na kusema alishiriki katika upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipande hicho cha sigara jikoni na chumbani kwa Wema anakohifadhi viatu na nguo.

Amedai kuwa bangi anaijua ikiwa shambani kwani aliwahi kuiona Shinyanga lakini ikiwa nje ya hapo hawezi kuitambua. Wema na wenzake wawili wanashtakiwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na walikamatwa Februari 4, mwaka jana
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: