Tuesday, 13 March 2018

Rc Ole-Sendeka apingana na Sumatra


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole - Sendeka amewaruhusu madereva wa bajaji Mkoani Njombe ambao walisimamishwa kufanya shughuli zao katika barabara kuu ya Njombe - Songea na kuruhusu bajaji kuongezwa mpaka bajaji 100 kutoka 55 ambazo zilikuwepo.
Sendeka ameruhusu kufanya kazi bajaji baada ya kusimamishwa na mamlaka ya usafirishaji wa Majini na Nchi kavu Sumatra ambapo walisimamishwa kwa mujibu wa sheria ya bajaji na pikipiki ya mwaka 2010.
Aidha Madereva hao wa bajaji  wamedai kuwa walipeleka katika vituo ambavyo wanadai kuwa havikuwa na maslahi kwao na kwa biashara yao na hakukuwa rafiki kimiundombinu.
Hata hivyo wamiliki wa bajaji Mjini Njombe wamesema kuwa kwa muda wa wiki moja hawajaingiza fedha yoyote na kusema serikali imefanya vyema kutoa maamuzi hayo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: