Thursday, 8 March 2018

Rc Mnyeti Atengua kauli ya Waziri Dr. Kigwangala


Mgogoro wa ardhi kati ya pori  tengefu la mkungunero hifadhi ya Tarangire na wakazi wa kijiji cha kimotorok wilaya ya simanjiro umechukua sura mpya baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa manyara kufika katika eneo ilo na kutoa siku kumi kwa wataalam wa ardhi kuhakiki upya alama za mipaka.

Baada ya kufika katika eneo ilo kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Manyara ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Manyara Alaxander Mnyeti  ilikagua mipaka  na kupata maelezo kutoka kwa wananchi  kisha ikatoa agizo ilo  la kuwataka wananchi kutokundoka katika eneo mpaka uhakiki wa mipaka utakapofanyika upya kutoka idara ya ardhi ambalo katibu tawala msaidizi mundombinu  wa mkoa huo bi suma tukampele mwakasitu anaahidi kuyatekeleza kwa umakini mkubwa maagizo hayo.                      


kwa upande wao wakazi wa kijiji  cha kimotorok  walipata nafasi ya kutoa madukuduku yao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Manyara wanasema hawawezi kuondoka katika eneo kwani wamekaa tangu mwaka sabini na mbili na mipaka ya hifadhi ya tarangire wanaijua lakini wanshangaa kwanii wameongeza mipaka hyo huku Mbunge  wa simanjiro James  ole Milya akiwataka wataalamu hao kufanya uhakiki bila kupendelea upande wowote.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: