Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti  ameliwezesha  jeshi  la polisi  mkoani humo kwa kuwapa  matairi nane kwa lengo  la kuendasha doria za kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amelitaka jeshi hilo kutumia vifaa hivyo kwa haraka ili wasiipe hasara serikali ya kupoteza askari watendaji pia kutoa taarifa pindi watakapoona hitilafu yoyote kwenye vyombo hivyo vya moto na kuwahidi kuendelea kuongeza tairi zingine ili kazi ya ulinzi izidi kuimarika.
Tairi hizo zinakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni mbili laki moja na elfu sitini zimetolewa kwa lengo  la kuendesha doria za kupambana na uhalifu.
"Ambacho hatutaki ni, mwenyekiti wa kitongoji alalamike, wa kijiji alalamike na ye mtendaji wa kata alalamike halafu tuwasikie na nyie mnalalamika haipendezi, polisi wanapaswa kufanya kazi. Serikali ni kubwa na ina wadau wengi wapo watatusaidia na tutapata tairi nyingine. Tunawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya." Mnyeti.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: