Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi likimalizana na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo wamlete Dar es Salaam kwani amedai haiwezekani akauchafua mkoa wake wa Dar es Salaam
Paul Makonda amesema hayo leo na kuwataka waandishi wa habari kutoandika habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika kwani wanaweza kupelekea taarifa kwa umma ambazo zinaweza kuleta taharuki kwa Umma.
"Juzi nimesikia sikia mmoja anasema ametekwa mimi nafikiri wakimalizana naye kule Iringa watuletee hapa Dar es Salaam, asituchafulie mkoa wetu na wengine wanaokimbia kuandika andika bila hata kuwa na ushahidi kwamba mtu ametekwa, wewe watu wamefunga chuo wanarudi majumbani kwao hata ikipotea network njiani fulani hatumuoni ametekwa ita waandishi wa habari toa kauli ifike hatua niwaombe waandishi wa habari angalieni taarifa mnazopeleka kwa Umma kama hazijathibitishwa na mamlaka husika achaneni nazo tusitengeneze taarifa ambayo ikifika kwa Umma inaleta taharuki isiyokuwa ya msingi" alisema Paul Makonda 
Abdul Nondo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha akiwa jijini Dar es Salaam na baadae kuripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana lakini alikuja kupatikana mkoani Iringa ambapo imedaiwa alitupwa huko, jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa kwa kijana huyo. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: