Saturday, 10 March 2018

Rc makonda : Maandamano watafanya nikiwa nimeondoka


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema watu wanaojifanya kutaka kuandamana wataweza kufanya hivyo kipindi ambacho yeye hatakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au hakiwa ameondoka ila vinginevyo hawawezi kuthubutu kuandamana.
Makonda amesema hayo akiwa anahotubia kwenye moja ya mkutano uliofanyika Dar es Salaam na kusema kuwa watu wengine ambao wanapiga sana kelele kuhusu maandamano hayo na kutaka kuvuruga amani ya nchi ndiyo wanapata fedha nyingi kutoka wa wafadhili wao ambao hawataki Mkoa wa Dar es Salaam ubaki salama. 
"Kuna kakundi hapa kanahangaika kweli usiku na mchana wengine wanahangaika kutumia mitandao ya kijamii kutukana viongozi, kuhamasisha sijui wanaita nini sijui maandamano nawapa pole sana, watafanya labda mimi nikiondoka nikiwa siyo Mkuu wa Mkoa kwenye huu Mkoa hiyo mipango mipango yao watafanya labda mimi nikiwa sipo lakini amani ya mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana" alisema 
Makonda aliendelea kudai kuwa 
"Amani ni muhimu sana kuliko propaganda za kisiasa na niwaambieni tu wengine wakipiga kelele na kutokea kwenye 'front page' kwenye magazeti ndiyo wanapata mshahara zaidi, wanapata donor kutoka kwenye baadhi ya mataifa yasiyotakia amani taifa letu kwa hiyo lazima tujue tunaye adui tunayeishi naye kama Mtanzania lakini amebeba majukumu ya mataifa yasiyoitakia amani taifa letu" alisisitiza Makonda
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: