Sunday, 18 March 2018

RC MAKONDA KUVITAJIRISHA VIKUNDI VYA JOGGING DARMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza mpango kabambe wa kuviwezesha vikundi vya mazoezi ya kukimbia (Jogging club) kwa kuweka utaratibu wa mashindano ya ya kila Mwisho wa Mwezi ambapo kikundi kitakachoshinda kitapatiwa kiasi cha shilingi Million 10 Kama mtaji wa kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kubaini idadi kubwa ya vijana hao wakimaliza mazoezi asubuhi hawana shughuli za kufanya hivyo wanakaa vijiweni na kitendo cha kukaa kijiweni wanaweza kushawishika kufanya vitendo vya uhalifu hivyo kwa kuwapatia mtaji itawawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali utakaowakwamua kiuchumi.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: