Thursday, 29 March 2018

RC MAKONDA ATOA ZAWADI KWA WAJAWAZITO WATAKAOJIFUNGUA PASAKA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka.

Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo.

RC Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya RC Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dr. Grace Maghembeamesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Vifaa hivi vinapatikana Bure kwenye Hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa Msimu huu wa Pasaka hivyo kwa wewe Mama unaetaka kujifungua fika Hospitalini vifaa vyako utavikuta.

KUTOA NI MOYO, SIO UTAJIRI
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: