Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Machi 26, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 ambayo yatakuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imeweka wazi kuwa Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari hayo 181 yaliyopo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

"Mageuzi Sekta ya Afya yanaendelea, usikose hafla ya kupokea magari mapya 181 kufikisha dawa na vifaa tiba zaidi mijini na vijijini" alisema Dkt Abass
Share To:

msumbanews

Post A Comment: