Thursday, 8 March 2018

Rais Magufuli: Daima tutaendelea kuwaheshimu wanawake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza wanawake wote duniani na kuwatakia kheri katika siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi,8 ya kila mwaka.
Rais Magufuli kuupitia mtandao wa kijamii wa Twitter,ametoa salamu hizo huku akisihi jamii kuwaheshimu wanawake na kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi za wanawake katika jamii yetu.

Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: