Ombaomba wakabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa - MSUMBA NEWS BLOG

Monday, 19 March 2018

Ombaomba wakabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kubuni mikakati ya kuondoa tatizo la ombaomba mijini.
Mh. Jafo amesema hayo alipokuwa akizindua Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam ambao umelenga kuvutia watalii mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya jiji hilo.
Katika uzinduzi huo, Jafo amesema ombaomba hao wamekuwa wakikaa barabarani hali ambayo haileti sura nzuri kwa nchi na kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii nchini.
Aidha, amebainisha kuwa, changamoto ya watoto wa mitaani na tatizo kubwa la ombaomba ni vyema wakuu hao wakabuni mbinu mbalimbali zikiwemo za kuwawekea maeneo maalum ya kujihusisha na shughuli za ufugaji na kilimo cha bustani ili kuwaondoa mitaani.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done