NUH MZIWANDA AANIKA MJENGO WAKE


MSANII wa Bongo FlevaNuh Mziwandaameonekana kukerwa na baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakidai kuwa amefulia tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni mwanamuziki,Zuwena Mohammed ‘Shilole’.

Nuh amewajibu watu hao kwa vitendo huku akianika mjengo wake mpya ambao upo eneo la Kivule nje kidogo ya jiji la Dar.

Nuh Mziwanda kupitia  ukurasa wake wa Instagram ameandika.

“Mjini wengi wajanja wao sisi wajinga daily, hatuna mipango ila kila mafanikio yapo moyoni mwa mtu acha tuendelee kuchorana tu. Hii hapa ya mwanangu Anya kwa nguvu za Mungu imefikia hapo Kivule moja. Endeleeni kumzungumzia Nuh halafu mie nafanya wonders.”
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: