Sunday, 18 March 2018

Nilitamani sana nimuone rafiki yangu Nondo – Waziri Mwigulu Nchemba


Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya kwa serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya huku akieleza alivyotamani kumuona Nondo.
Mwigulu ameyasema hayo kwenye kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum Ester Mmasi, ambapo amesema alitamani kumuona mwanafunzi aliyedaiwa kutekwa hivi karibuni Abdul Nondo.
”Acheni kufanya ‘Student Movement’ na kujifanya maadui wa serikali, mimi nimewahi kufanya hivyo tena sikuhizi zimepoa lakini sio hii ya kutaka kutengeneza picha mbaya kwa serikali, kama rafiki yangu Nondo nilitaka sana leo nimuone hapa”, amesema Mwigulu.
Aidha Mwigulu ameeleza kushangazwa na kitendo cha mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kutamka kuwa waziri ajiuzulu, akienda mbali zaidi kwa kusema yeye alidhani anamaanisha waziri wa serikali za wanafunzi na sio yeye ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani.
Kwa upande mwingine Mwigulu amewaasa wanafunzi kuwa wema chuoni kwani kuwa kijana mwema chuoni, sio kwa kuwa kimya bali kuwa na mitazamo chanya ambayo itasaidia kujenga na kuboresha mambo mbalimbali ya serikali.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: