Wednesday, 7 March 2018

Nassari ataka wananchi kupewa mbadala wa zao la bangiMbunge wa Arumeru Mashariki (Chademap), Joshua Nassari ameitaka Serikali kuwapatia  zao mbadala wananchi wa jimbo lake ambao baadhi wamekuwa wakitegemea kulima bangi kama zao za biashara.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Arusha(RCC) leo Jumatano Machi 7, 2018 Nassari amesema wananchi hasa maeneo ya Kisimiri hawajui kilimo kingine cha biashara  zaidi ya bangi.
"Magunia mengi ya bangi yamekamatwa katika jimbo langu, lakini tulikubaliana kikao kilichopita cha RCC wananchi watafute zao mbadala walime hasa Pareto lakini hadi sasa hawajafundishwa kulima,”amesema.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa Arusha, Iddi Kimanta amesema kulima bangi ni kosa la kamwe Serikali haitawavulia.
Amesema bodi ya Pareto imeahidi kuanzia Machi itaanza kutoa elimu hivyo Nassari awe na subira.
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe akichangia hoja amemtaka Nassari kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufikia uamuzi kuwatafutia zao mbadala wananchi wa Meru.
"Nassari ashukuru sana  Serikali kwani ingeweza kupiga marufuku kilimo cha bangi kama madawa ya kulevya mengine bila kutoa mbadala" amesema.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: