Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema Tanzania hakuna tishio lolote kuhusu watu kupotea au kuuawa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kusema kuwa Wizara yake inapambana kuhakikisha watu na mali zao wako salama.

Waziri mwigulu Nchemba alisema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na kudai kuwa miili ya watu ambayo imekuwa ikiokotwa baharini si miili ya Watanzania kwani kama ingekuwa miili ya Watanzania hivyo basi familia zao zingekuwa zinasikika kizipiga kelele kuhusu ndugu zao hao kupotea.

"Mimi kama Waziri wa Mambo ya Ndani nakuhakikishieni Watanzania kwamba Wizara inapambana kuhakikisha watu na mali zao wako salama na mpaka sasa hakuna tishio la namna hiyo kusema kwamba watu wanapotea hovyo hovyo au watu wanauawa hakuna kitu cha namna hiyo, inatokea miili inaokotwa baharini bahari ambayo tunachangia na nchi nyingi sana na miili inaweza kusafiri kwa upepo kutoka sehemu nyingi sana lakini kuna watu wanasema watu wanauawa hovyo, haiwezekani watu wauawe hovyo halafu kukawa shwari tu familia zikawa zimetulia lazima familia zingepiga kelele" alisema Mwigulu Nchemba

Aidha Waziri Mwigulu Nchemba ametaka ajenda za watu zisigeuke kuwa siasa na kusema kuwa ajenda za siasa zifanywe kwenye siasa na si maisha ya watu pia Mwigulu Nchemba amedai kuwa katika matukio rasmi ambayo wao waliyapata ni kuhusu kutekwa kwa watoto Arusha.

"Utekwaji wa watoto ni jambo ambalo lilikuwa serious Watanzania wote waliona na wahalifu wakakamatwa ni bahati mbaya tu tulikuja kuwakamata na kuokoa mtoto mmoja yule lakini wengine wale walikuwa wameshawadhuru lakini tuliweza kuwakamata na kukamata ule mtandao ndiyo maana ile hali ilitulia na naendelea kuwataka Watanzania kuwa makini kwa sababu suala la usalama ni jambo ni endelevu" alisema Mwigulu Nchemba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: