Wednesday, 14 March 2018

Mwalimu afariki baada ya kupewa barua ya uhamisho


Mwalimu Mathew Clement wa shule ya Sekondari Milongodi iliyopo wilayani Tandahima Mkoani Mtwara, ambaye ni mwenyeji wa Kilosa mkoani Morogoro, amefariki dunia kwa shinikizo la moyo baada ya kupewa uhamisho wa kwenda kufundisha shule ya msingi.
Kwenye taarifa iliyotolewa na Mkiti CWT (W) Kilosa Bwana Mussa Mnyeti, imesema kwamba Mwalimu Clement amefariki ghafla baada ya kupata presha, siku moja baada ya kuitwa na kupewa barua ya uhamisho wa kwenda kufundisha kutoka shule ya sekondari na kwenda kufundisha shule ya Msingi.
Taarifa zaidi zinasema kwamba mwalimu Clement licha ya kupata presha hiyo, pia alikataa kupokea barua ya uhamisho huo.
Mwili wa marehemu tayari umeshasafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi na taarifa zinasema kwmaba mwalimu huyo ameshazikwa, huku akiwa ameacha mke na watoto wawili.
Hivi karibuni serikali imeanzisha mfumo wa kuhamisha walimu wa sekondari na kwenda kufundisha shule za msingi, ikiwa na lengo la kukidhi uhaba wa walimu na kuboresha elimu ya msingi, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na baadhi ya walimu waliokumbwa na sakata hilo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: