Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaitumia Azam FC kama njia na kusonga mbele katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa.


"Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana na tuko Dar es Salaam kutafuta matokeo ya mechi hiyo," alisema.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu hizo ambao wamekuwa wakiuonyesha katika mchuano hiyo na Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mshindi katika mechi hiyo ataingia nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: