Friday, 16 March 2018

Msanii Wema Sepetu amwagia sifa Diamond

Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amemwagia sifa msanii wa muziki Diamond Platnumz.
Wema amemwagia sifa Diamond ambaye ni Boss wake na kusema kuwa anaweza na anajua, hii ni baada ya msanii huyo kuachia video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘African Beauty’ aliyomshirikisha msanii wa muziki kutoka Marekani aliyekuwa katika kundi la B2K Omarion.
“All dat Said…Let’s get back to Reality…. Chibu, Unaweza…!!!Chibu, Unajua….!!! Keep Doin wat you do and Live Your Dream… Bonge moja la Track… Na Hongera kwa kummezesha Omarion Swahili… I can imagine kazi uliokuwa nayo… Salute kwako…,” ameandika Wema katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
African Beuty ni moja ya ngoma inayopatikana katika albamu yake ya pili ya A Boy From Tandale
Machi 11 mwaka huu, Wema alijibu tetesi za kutaka kuolewa na Diamond pia alielezea ujio wa kipindi chake cha Tv kupitia Wasafi TV.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: