Mke wa Roma Mkatoliki afunguka mazito


Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka na kuweka wazi kuwa mume wake Roma Mkatoliki anapitia katika wakati mgumu sana kuhusu muziki wake na maisha ya muziki kiujumla kiasi cha kutamani aache muziki. 
Mke wa Roma ambaye juzi amejifungua mtoto wake wa pili amesema hayo wakati akimshukuru Vanessa Mdee baada ya kumuona akimpigania mumewe kuhusu sanaa yake na kusema kuwa Roma Mkatoliki amekuwa akipitia magumu lakini kinachomshangaza zaidi kwanini yote hayo yanamkuta yeye tu. 
"Mungu akubariki Wifi yangu Ahsante sana Vanessa Mdee ila mume wangu anakutana na nyakati ngumu na changamoto sana kwenye muziki wake, hadi kuna wakati natamani uache muziki, ila najiuliza kwanini kila siku wewe tu? Haina tatizo endelea kupambana kwani hata hili litapita" alisema Mke wa Roma Mkatoliki 
April 5, 2017 rapa Roma Mkatoliki alitekwa na watu wasiojulkana akiwa katika studio za Tongwe Records ambapo alikuja kuonekana baadaye akiwa na majeraha mwilini mwake huku kidole chake kikiwa kimevunjwa, lakini Machi 1, 2018 Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni imemfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za muziki kwa kipindi cha miezi sita kutokana na kukaidi kufanyia marekebisho wimbo wake wa 'Kibamia'
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: